Africa Pension Fund (APeF) inakuletea wewe mwekezaji mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulioambatanishwa na faida ya bima ya maisha na ulemavu wa kudumu unaowekeza kwenye masoko ya fedha na dhamana. Mfuko huu umeundwa kuwapa wawekezaji fursa ya kukuza mitaji yao huku wakipata ulinzi wa bima ya maisha. Mfuko huu unakupa ulinzi wa mtaji, faida shindani, upatikanaji wa fedha kwa urahisi (ukwasi) pamoja na ulinzi wa bima ya maisha.
Mfuko huu unawekeza kwenye hatifungani za serikali za mda mrefu na mfupi, hatifungani za makampuni binafsi pamoja na amana za muda mfupi na za kudumu (call account & fixed deposits)..
Kigezo: Hatifungani za serikali za miaka miwili
Watu binafsi, pamoja na taasisi, kampuni, vyama na makundi yanayotaka kuweka mtaji wao kwa muda mfupi, huku wakilinda mtaji mkuu, kuhakikisha usalama, na kupata faida bora zaidi
At least 18 years. Minors under 18 can invest through a parent or guardian.
Valid ID: NIDA, Passport, Driver's License or Voters ID.
Minimum deposit of TZS 50,000 for account opening.
Tanzanian or SADC resident.
Ziada Fund inatoa mbadala wa kisasa kwa amana za benki kwa wawekezaji wa muda mfupi na mrefu. Lengo lake ni kutoa faida shindani na thabiti na kutoa kipaumbele kwenye ulinzi wa mtaji kupitia uwekezaji uliogawanywa katika soko la fedha na dhamana za muda mfupi.
Mfuko huu una ukwasi wa hali ya juu, ukiruhusu kutoa sehemu ya mtaji ama mtaji wote, huku maombi ya kutoa fedha yakichakatwa ndani ya siku tatu za kazi. Hakuna ada za kuingia au kutoka, hivyo kuhakikisha upatikanaji wa mtaji bila gharama.
Vipande vya mfuko wa Ziada vinaweza kukubaliwa na taasisi za kifedha kama dhamana ya kupata mikopo, kulingana na tathmini ya mkopo ya mkopeshaji na masharti husika.
Wawekezaji pia wana fursa ya kuongeza uwekezaji wakati wowote, uchapishaji wa kila siku wa Thamani Halisi ya kipande (NAV), pamoja na mfumo kamili inayosimamiwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Faida za bima ya Maisha (Kupitia Alliance Life Assurance):
Earn competitive interest rates through a diversified money market portfolio.
Protection for investors with over TZS 250,000 NAV balance through Alliance Life.
Invest instantly via USSD *150*74# or the APeF mobile app — right where your money is.
Access your funds anytime, anywhere via our mobile app and web portal.
| Mauzo ya awali | 26 Januari 2026 |
| Kufunga Mauzo ya Awali | 13 Machi 2026 |
| Bei ya kipande | TZS 100 |
| Kiwango cha chini ya uwekezaji | TZS 50,000 |
| Uwekezaji wa unaofuata/baadae | TZS 10,000 |
| Kiwango cha chini cha uwekezaji ili kunufaika na Bima | TZS 250,000 |
| Tarehe ya Kuanza kwa Hati ya Bima | 26 Januari 2026 |